Menu

Yoshua 12

BIB

1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba: 2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi ), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga. 4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. 5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni. 6 Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao. 7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 8 nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi): 9 mfalme wa Yerikommojamfalme wa Ai (karibu na Betheli)mmoja 10 mfalme wa Yerusalemummojamfalme wa Hebronimmoja 11 mfalme wa Yarmuthimmojamfalme wa Lakishimmoja 12 mfalme wa Eglonimmojamfalme wa Gezerimmoja 13 mfalme wa Debirimmojamfalme wa Gederimmoja 14 mfalme wa Hormammojamfalme wa Aradimmoja 15 mfalme wa Libnammojamfalme wa Adulamummoja 16 mfalme wa Makedammojamfalme wa Bethelimmoja 17 mfalme wa Tapuammojamfalme wa Heferimmoja 18 mfalme wa Afekimmojamfalme wa Lasharonimmoja 19 mfalme wa Madonimmojamfalme wa Hazorimmoja 20 mfalme wa Shimron-Meronimmojamfalme wa Akishafummoja 21 mfalme wa Taanakimmojamfalme wa Megidommoja 22 mfalme wa Kedeshimmojamfalme wa Yokneamu katika Karmelimmoja 23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmojamfalme wa Goimu katika Gilgalimmoja 24 mfalme wa Tirsammoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate