Menu

Zaburi 120

BIB

1 Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. 2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. 3 Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? 4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6 Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. 7 Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate