Menu

Zaburi 46

BIB

1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 2 Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. 3 Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. 4 Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. 5 Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. 6 Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka. 7 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 8 Njooni mkaone kazi za Bwana jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. 9 Anakomesha vita hata miisho ya dunia, anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, anateketeza ngao kwa moto. 10 “Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; nitatukuzwa katikati ya mataifa, nitatukuzwa katika dunia." 11 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate