Menu

Zaburi 87

BIB

1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ “ 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha." 6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni." 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako."

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate