Menu

Zaburi 23

ONMM

1 Mwenyezi Mungu ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 2 Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, 3 hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Hata nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji. 5 Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu milele.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate