Menu

Zaburi 15

ONMM

1 Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? 2 Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake, 3 na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake, 4 ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. 5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate